

소개
Vigelegele, vifijo na cherekochereko za kina mama wakiimba mamie mwana so ukaule mgeni kengia ndizo zinazokamilisha kilele cha harusi ya Rahman, mtoto wa Alhaj Mwinyi Karim kwa Shufaa binti wa Mwinyi Sitaki Shari. Hakuna kinachokosekana siku hiyo. Fahari yote na utajiri wa Alhaj Karim ulitengwa kukamilisha ndoa hiyo ili iwe harusi ya kusimuliwa.



