소개

Fumo Liongo alikuwa shujaa wa mji wa Pate katika Pwani ya Afrika ya Mashariki aliyeishi kati ya karne ya 9 na 13.Umaarufu wa Fumo Liongo ulitokana na ushujaa, uzalendo na kipaji chake cha umalenga miongoni mwa watu wa Pate na maeneo ya jirani. Kwa Mfalme Mringwari, ushujaa na umaarufu wa Liongo ni tishio kubwa dhidi ya utawala wake. Kilele cha hofu na chuki dhidi ya Fumo Liongo kinafikiwa pale Liongo anapoliongoza jeshi vitani na kuwashinda Wagala, maadui zao wa jadi.